Diamond aanza mipango ya harusi kimyakimya

Monday April 22 2019

 

HUKU stori za ndoa za  staa wa Bongo Flava Diamond Platinumz na mpenzi wake, Tanasha Donna zikiwa zimefifia kwa sasa baada ya kuahirishwa, dada yake kazifufua tena.

Mwaka jana wakati kukiendelea na maandalizi ya Wasafi festival, Diamond alifrichua kwamba angefunga ndoa na mpenzi wake Tanasha Februari 14 ya mwaka huu.

Lakini  siku chache baadaye alitangaza kuahirisha mipango hiyo hadi siku nyingine ambayo hakuiweka wazi.

Wadau wengi wakaishia kujijazia kuwa, kauli hiyo ilikuwa kwa ajili ya kuipa kiki Wasafi Festival na wala hapakuwepo na lolote.

na huku mashabiki wakionekana kulisahahu, dadake mkubwa Diamond ambaye ni mtu wa karibu sana naye, ukimgusa unakuwa umemumiza msanii huyo, kaamka na kutoa nzito akisisitiza kuwa mipango ya kimyakimya kwa ajili ya harusi hiyo inagali inaendelea.

“Sasa si yule ndio wife wa kaka yangu jamani, hakuna kubadilisha hilo na ndoa ipo kama kawaida tujipange tu kusherehekea na vigoma vya Kigoma” alinukuliwa Esma Khan.

Advertisement

Kulinganan na Esma, kilichosababishia tarehe mpya kutotangazwa ni kwa sababu  kaka yake pamoja  na wifi yake wana ratiba finyu ya kikazi na kuwa masuala ya  harusi yanahitaji muda mwingi wa karibu, ila yote tisa, kumi wangali wanalifanyia kazi.

Advertisement