Diamond Platnumz, Tanasha waibuka na wimbo Gere

Muktasari:

Video ya wimbo huo imeiachia saa tatu zilizopita ikiwa ni mara ya kwanza Diamond kuimba pamoja mpenzi wake huyo

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platinumz ametoa wimbo mpya akiwa na mpenzi wake Tanasha Donna inayoitwa 'Gere' ndani ya saa tano imepata watazamaji 327,006 katika youtube.

Diamond na Tanasha wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Nassibu, video yao hiyo wameiachia saa tano zilizopita ikiwa ni mara ya kwanza Diamond kuimba na mpenzi wake huyo.

Wimbo huo ulifanywa na Producer Lizer kutoka WCB na video yake kufanywa Director Kenny kutoka Zoom Production inayosimamiwa na Diamond, imezua taharuki kwenye mtandao wa Instagram, baada siku kadhaa zilizopita kulikuwa na madai ya Diamond na Tanasha wameachana.

Watu wa Instagram waliendelea kutoa madai ya kuachana kati ya wawili hao kuwa baada ya Tanasha kumkuta na mwanamke Diamond hotelini kipindi cha uzinduzi wa EP iliyoandaliwa na Tanasha mjini Nairobi saa chache kabla ya uzinduzi kuanza.

Baadae Dimond aliweka wazi sababu ya kuondoka kutohudhuria uzinduzi wa mpenzi wake huyo ni alipata dharura ya kifamilia hivyo asingeweza kupata nafasi ya kurejea kuungana naye katika uzinduzi huo.

Video ya wimbo wa Gere ni kama vijembe kwa watu wanaowafuatilia penzi lao na kutaka waachane.