Davido amvisha pete Chioma

Friday September 13 2019

 

By Ramadhan Elias, Saut

NYOTA wa muziki nchini Nigeria David Adedeji Adelelee maarufu kama Davido, amemvisha pete ya  Uchumba mpenzi wake wa muda mrefu Chioma Avril Rowland maarufu kama Chef chi.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa picha (instagram), Davido (@davidoofficial ) ameweka picha na video ambazo zinaonesha mkono wake na mkono wa mpenzio wake akiwa ameivaa pete hiyo.

Pia Davido ameweka wazi  furaha yake kukamilisha jambo hilo kumbwa katika maisha na kuweka wazi kuwa Atafunga ndoa na mpenzi wake huyo mwaka 2020.

Chioma amnezaliwa Aprili 1,1995 (24), huku mpenzi wake Davido akiwa amezaliwa Novemba 21,1992 na mwezi huu atafikisha umri wa miaka 27.

Advertisement