Cheki Neres alivyotongoza demu kibabe

Thursday May 23 2019

 

By Thomas Matiko

KINDA winga mahiri wa Ajax, David Neres anayeripotiwa kumezewa mate na miamba PSG, Liverpool na Borussia Dortmund kafichua alimtongoza mpenzi wake kiujeuri kupitia DM.

Neres ambaye mabao yake yalichangiwa kuwabandua miamba Real Madrid na Juventus kwenye kinyang’anyiro cha Champions League msimu huu, kafichua alimtongoza demu wake mwanamitindo Mjerumani, Kira Winona kwa kumtumia meseji kwenye Instagramu yake anamtaka.

“Sikujua wanawake wa Kijerumani kumbe wanawapenda watanashati wa Kibrazil. Nilimkuta Instagramu nikamtumia ujumbe kwenye DM mimi ni David Neres njoo kwangu. Hilo lilitosha yeye kunipa deti,” Neres akafichua.

Kinda huyo mwenye miaka 22 msimu huu kapachika mabao 15 na kutoa asisti 14, mchango uliowawezesha Ajax kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi.

Advertisement