Ali Kiba aanika sababu za kukacha Wasafi Festival

Saturday November 9 2019

 

By Rhobi Chacha

NYOTA wa kimataifa na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametaja sababu ya kukataa kushiriki Tamasha la Wasafi Festival 2019 lililoandaliwa na Kampuni ya Wasafi media chini ya Mkurugenzi Nassibu Abdul 'Diamond Plutnumz'
Amesema  hana ugomvi na Diamond, ila hawezi kushiriki kwenye matamasha ya muimbaji huyo kwa kuwa naye anashughuli zake nyingi za kufanya.
Maneno hayo amesema jana jioni jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari  akitangaza ujio wa Ali Kiba Unforgettable Tour.
Aidha Kiba amefafanua maneno aliyoandika Octoba 30, 2019 katika Akaunti yake ya Instagram aliyokuwa ameandika:
"Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME)
Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema
#KingKiba" baada ya kutajwa na Diamond kuwa atashiriki katika Tamasha la Wasafi Festival.
Amefafanua kuwa hakumaanisha amepoteza penseli kama baadhi ya watu wanavyodhani  bali aliongea maneno ya kikubwa zaidi ili Diamond platnumz aelewe, Sababu  alishamwambia hawezi kuperfom kwenye Matamasha yake lakini yeye alirudia kuongea neno hilo hilo.
Aidha Ali Kiba amesema  mwisho wa mwaka huu anatimiza miaka 17 kwenye Tasnia ya Muziki, hivyo lengo la Ali Kiba Unforgettable Tour ni kulipa deni kwa mashabiki zake kwa kumsapoti miaka yote hiyo.

Advertisement