Mzee Yusuf kuachia wimbo wa kwanza leo

Saturday August 1 2020

 

By Nasra Aabdallah

Siku chache baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki, Msanii wa taarabu Mzee Yussuf natarajia kuachia wimbo wake wa kwanza leo.

Hii ni baada ya kuwa nje ya tasnia hiyo kwa takribani miaka minne ambapo mwaka 2016 alitangaza kuacha kuimba taarabu na kujikita katika shughuli za ualimu wa dini na kutoa dawa.

Hata hivyo Machi 12 mwaka huu aliwashtua wengi pale alipoandika kwenye ukurasa wake kwenye mtandao Instagram kuwa anarudi mjini na ataimba mpaka agalegale na wiki iliyopita alipohojiwa alifunguka kuwa anarudi rasmi kwenye muzik.

Anafanya hivyo akiwa katika maandalizi ya onyesho lake lililokuwa lifanyike jana sikuu ya Eid lakini lilisogezwa mbele kutokana na msiba wa Rais Mstaafu awamu ya tatu,Benjamin Mkapa ambalo sasa linatarajiwa kufanyika mkesha wa kuamkia sikukuu ya nanenane.

.Katika ukurasa wake ametangaza kuachia wimbo wake huo leo unaokwenda kwa jina Najilipua kwa kuandika ‘Najilipua itakuwa hapa masaa machache,”.

Hii inahitimisha safari yake ya kurudi kwenye muziki, kwa kuachia wimbo wa kwanza tangu alipoacha kuimba.

Advertisement

Advertisement