Vigogo wamwagika jela kumtembelea Meek Mill

Friday April 13 2018

 

KAMA wakishindanishwa wafungwa wanaotembelewa na watu wazito kwa sasa, Meek Mill anaweza kuongoza.

Tangu ahukumiwe kifungo cha miaka miwili jela, rapa huyo amekuwa akitembelewa na watu mbalimbali maarufu nchini Marekani.

Hivi karibuni, meya wa Philadelphia Jim Kenney alikuwa miongoni kwa wageni waliomtembelea rapa huyo.

Kenney aliambatana na mmiliki wa timu ya 76ers Michael Rubin ambaye amekuwa akimtembelea Meek mara kwa mara.

Msemaji wa Meya huyo alisema Kenney anaamini kuwa Meek angeweza kutumikia adhabu yake nje kuliko ilivyofanywa sasa.