Tabu kuelimisha jamii kupitia sanaa

Muktasari:

Wasanii wameshauriwa kutumia sanaa kuelimisha jamii inayowaunga juu ya kuelewa namna ya kujikinga na maambukizi ya corona.
 

MSANII wa vichekesho nchini, Tabu Mtingita amesema anatumia sanaa yake kuelimisha jamii namna ya kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Corona, akiamini atawafikia kwa uharaka.
Amesema kama jamii inamfuatilia katika vichekesho vyake ameamua kuipelekea ujumbe kwa njia ya kuigiza ili waweze kuchukulia uzito suala hilo.
"Ni jukumu la kila Mtanzania kukumbushana na kuelimishana jinsi ya kujiweka salama na haya maambukizi ya virusi vya Corona kwamba huu ni ugonjwa hatari na unatikisa dunia,"amesema.
Hivi karibuni Tabu ametoa kichekesho kinachozungumzia juu ya tahadhari ya Corona, akiwashauri wapenzi kutokumbatiana hovyo kipindi hiki.
"Wasanii tuna nafasi kubwa ya kuwafikia jamii, tuna watu wengi wanaotuangalia kwenye kazi zetu ni vyema tuanze na hao nao wataenda kuwafikishia wengi naamini Tanzania tutakuwa tumepona,"amesema.