Manara aishukia Yanga

Monday February 27 2017

 

By Fredrick Nwaka, Mwananchi; fnwaka@mwananchi.co.tz

Dar es salaam.Uongozi wa klabu ya Simba umewapongeza waamuzi waliochezesha mchezo wake dhidi ya Yanga na kuwakejeli watani zao hao kuwa hawawasumbui kwa sasa.

Ofisa Habara wa Simba, Haji amesema kauli za viongozi wa Yanga zimewaponza kwa timu yao kufungwa mabao 2-1.

"Klabu imeridhishwa na kiwango cha waamuzi, sisi hatutaki kubebwa tunataka fair play, lakini zaidi tumewafunga mdomo hasa huyo Mkemi (Salum)."

"Nilikuwa kimya nikimsikiliza, lakini majibu ameyapata, tumewapiga mbili saafi Simba ni klabu kubwa," amesema.

Msemaji huyo ameongeza licha ya kutoipuuza Yanga, lakini hawana muda nayo kwakuwa wameshamiria kutwaa ubigwa wa Ligi Kuu.

"Tutatumia nguvu ile ile kwenye mechi zilizobaki, tunakutana na Mbeya City haituidharau tutaipiga kama tunacheza na mkubwa mwenzetu," amesema Manara.

Advertisement

Simba inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 54, ikifutiwa na Yanga yenye pointi 49 ikiwa mchezo moja mkononi.

Advertisement