Saudi Arabia yaomba radhi kusahau kuomboleza ugaidi

Muktasari:

Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo ilisema, “Tunaomba radhi kwa kosa tulilotenda kutokana na wawakilishi wetu kusahau kuwa kimya kwa dakika kadhaa ili kuomboleza shambulio la London.”

 Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF), limeomba radhi kwa kusahau kuwa kimya kwa dakika kadhaa kama ishara ya kuomboleza shambulio la kigaidi lililotokea London kabla ya mechi yao timu yao ya taifa dhidi ya Australia.

Hata hivyo Saudi Arabia walilala kwa mabao 3-2 ikiwa ni mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwakani.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo ilisema, “Tunaomba radhi kwa kosa tulilotenda kutokana na wawakilishi wetu kusahau kuwa kimya kwa dakika kadhaa ili kuomboleza shambulio la London.”

Shambulio hilo lilitokea Juni 3 na kuua watu saba, huku wengine wakijeruhiwa. Tukio hilo lilikuwa la pil katika kipindi na jingine lilitokea Mei na kuua watu 22 huku zaidi ya 50 wakijeruhiwa.

Shirikisho hilo lilisema kwamba linapinga vikali vitendo vyote vya kigaidi na linaungana na wanafamilia wote wa walioathirika kwa namna moja au nyingine.