Real Madrid yaivurugia hesabu Manchester United

Wednesday August 9 2017

 

Klabu ya Real Madrid imeiduwaza Manchester United  baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuchukua taji la Super Cup, huku vijana wa Jose Mourinho wakikosa nafasi nyingi kwenye mchezo huo  uliofanyika jana Jumanne Skopje, Macedonia.

Hesabu za Mourinho zilikuwa kuukaribisha msimu mpya wa mwaka 2017/18 kwa taji jambo ambalo kikosi cha Real Madrid imelitibua mapema.

Romelo Lukaku ndiye aliiyeifungia bao Manchester United katika mechi hiyo ambayo walikuwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi.