Mwingereza Konta aaga mashindano ya Wimbledon, Venus atinga fainali

Friday July 14 2017

 

London, England. Mcheza tenisi mwanamke raia wa Uingereza aliyeweka rekodi wiki hii kufika hatua ya nusu fainali, Johanna Konta ameaga mashindano hayo baada ya kufungwa seti 4-6 2-6 na kumpa mwanya Venus Williams kusonga mbele.

Konta alivunja rekodi iliyowekwa tangu mwaka 1978 iliyowekwa na Virginia Wade.

Hivyo mkongwe huyo wa Marekani, Venus ataingia uwanjani kesho kwenye mchezo wake wa fainali.

Venus atakutana na Garbine Muguruza ambaye amekuwa na rekodi nzuri kwenye mchezo wa tenisi.