Mourinho hafurahii usajili unaofanywa na maofisa wa Manchester

Muktasari:

Man United imekamilisha dili za usajili wa wachezaji wawili tu, Victor Lindelof na Romelu Lukaku huku ikishindwa kunasa saini za wachezaji iliyohusishwa nao kuwasajili katika kipindi hiki.

London, England. Jose Mourinho amesema hafurahishwi na namna maofisa wa Manchester United wanavyofanya usajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Man United imekamilisha dili za usajili wa wachezaji wawili tu, Victor Lindelof na Romelu Lukaku huku ikishindwa kunasa saini za wachezaji iliyohusishwa nao kuwasajili katika kipindi hiki.

Man United iliripotiwa ingekamilisha usajili wa winga wa Inter Milan, Ivan Perisic wiki hii.