Mchezaji wa Dortmund aamua kustaafu soka akihofia kulipuliwa mabomu

Muktasari:

Milipuko mitatu ilielekea jirani na gari walilokuwa wakitumia wakati wakikaribia Uwanja wa Signal Iduna, huku Marc Barta alijeruhiwa mkono kutokana na shambulizi hilo.

Ujerumani. Beki wa Borussia Dortmund, Mathhias Ginter ametangaza nia yake ya kustaafu soka baada ya klabu yake kushambuliwa wakati wakijiandaa kwenda uwanjani kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Monaco mwezi Aprili.

Milipuko mitatu ilielekea jirani na gari walilokuwa wakitumia wakati wakikaribia Uwanja wa Signal Iduna, huku Marc Barta alijeruhiwa mkono kutokana na shambulizi hilo.

Mchezaji huyo amejitokeza na kuhoji hatima yake ya soka iwapo mashambulizi yanaelekezwa kwenye masuala ya soka, huku akisema ikibidi huenda akatangaza kustaafu soka.

“Mara nyingi nimekuwa nikifikiria kustaafu kucheza mpira, huwezi kuhatarisha maisha yako kwa mashambulizi ya aina kama hii. Ninataka kujiweka mbali na masuala ya soka. Ninatarajia kufanya hivyo,” alisema mchezaji huyo.