Mayweather, Pacquiao zinapigwa tena

Muktasari:

  • Mabondia hao wawili maarufu kabisa walikutana Mei 2015 huko Las Vegas, Marekani na Mayweather alishinda kwa pointi. Bondia huyo Mmarekani alituma video yake kwenye mtandao wa kijamii yenye maneno: “Narudi kupigana na Manny Pacquiao mwaka huu. Malipo mengine ya tarakimu tisa yanakuja.”

BONDIA Floyd Mayweather amesema atatengua uamuzi wake wa kustaafu na hivyo kurejea ulingoni kuzipiga na Manny Pacquiao baadaye mwaka huu.

Mabondia hao wawili maarufu kabisa walikutana Mei 2015 huko Las Vegas, Marekani na Mayweather alishinda kwa pointi. Bondia huyo Mmarekani alituma video yake kwenye mtandao wa kijamii yenye maneno: “Narudi kupigana na Manny Pacquiao mwaka huu. Malipo mengine ya tarakimu tisa yanakuja.”

Mayweather hajapigana pambano lolote tangu Agosti mwaka jana alipozipiga na Conor McGregor.

Amir Khan naye anamtaka Pacquiao baada ya kumshinda Samuel Vargas siku chache zilizopita.