Marcos Alonso ndo kama ulivyosikia

Muktasari:

Kutokana na adhabu hiyo, staa huyo wa kimataifa wa Hispania atakosa mechi muhimu sana ikiwamo ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Southampton hao hao na pia hatacheza kwenye mechi za Ligi Kuu England dhidi ya Burnley na Swansea City.

BEKI wa pembeni wa Chelsea, Marcos Alonso amepigwa kitanzi cha kufungiwa mechi tatu na chama cha soka cha England baada ya kumshambulia straika wa Southampton, Shane Long.

Kutokana na adhabu hiyo, staa huyo wa kimataifa wa Hispania atakosa mechi muhimu sana ikiwamo ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Southampton hao hao na pia hatacheza kwenye mechi za Ligi Kuu England dhidi ya Burnley na Swansea City.

Chelsea ilitarajia kumenyana na Burnley usiku wa jana Alhamisi.

Alonso alinaswa na picha za kamera akimkanyaga mguu straika Long katika mechi ya Ligi Kuu England iliyofanyika St Mary’s wikiendi iliyopita na Chelsea ilitokea nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2.

Kutokana na kukana kufanya tukio hilo, Alonso amejikuta akiongezewa mechi na sasa kufikia tatu baada ya FA kutupilia mbali madai yake.

Kocha Antonio Conte sasa anaweza kumgeukia Emerson Palmieri ili kuziba pengo hilo la Alonso, ambaye jina lake lilitajwa pia kwenye kikosi cha kwanza cha msimu hu kwenye Ligi Kuu England.