Madrid yampa Ronaldo ofa ya pesa kiduchu

Muktasari:

Mmoja wa waandishi wenye heshima kubwa huko Hispania, Manolo Lama, alidai Real Madrid imempa ofa ya mkataba mpya Ronaldo wenye thamanai ya Euro 25 milioni kwa mwaka kabla ya makato ya kodi, huku kukiwa na nyongeza nyingine ya Euro 7.5 milioni kulingana na bonasi.

MADRID, HISPANIA. REAL Madrid imemwekea mezani ofa ya mkataba mpya supastaa wake Cristiano Ronaldo, lakini shida ni mshahara wake bado umeachwa mbali sana na anaolipwa mpinzani wake, Lionel Messi huko Barcelona.

Mmoja wa waandishi wenye heshima kubwa huko Hispania, Manolo Lama, alidai Real Madrid imempa ofa ya mkataba mpya Ronaldo wenye thamanai ya Euro 25 milioni kwa mwaka kabla ya makato ya kodi, huku kukiwa na nyongeza nyingine ya Euro 7.5 milioni kulingana na bonasi.

Kwa uchambuzi wa mshahara huo ikiwa pamoja na bonasi yake ambapo umegawanywa ni kwamba, Ronaldo atavuna Euro 2 milioni kama Real Madrid itabeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Euro 1.5 milioni kama itabeba ubingwa wa La Liga, Euro 1 milioni kwa ubingwa wa Copa del Rey, Euro 1 milioni kwa Tuzo ya Ballon d’Or na Euro 1 milioni nyingine kwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa na Euro 500,000 akibeba Tuzo ya Mfungaji Bora, Trofeo Pichichi, huko Euro 500,000 ikiwa bonasi itakayotokana na idadi ya mechi atakazocheza kwa msimu ujao.

Mshahara wa Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 kwa sasa ni Euro 21 milioni kwa mwaka.

Staa huyo wa Kireno aliripotiwa kutofurahia na mshahara wake a huko Bernabeu kwa sababu ameachwa mbalimbali na mastaa Messi na Neymar na hilo ndilo linaloleta chokochoko ya kudai ataihama timu hiyo mwaka huu.