Kumbe Bayern Munich hawana utani kabisa

Muktasari:

Washambuliaji nguli Thomas Muller na Robert Lewandowski walishirikiana kufanya mauaji hayo kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Ujerumani.

Munich, Ujerumani. Timu ya Bayern Munich imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuichakaza Besiktas mabao 5-0.

Washambuliaji nguli Thomas Muller na Robert Lewandowski walishirikiana kufanya mauaji hayo kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Ujerumani.

Muller na Lewandowski kila mmoja alifunga mabao mawili na moja lilifungwa na Kingsley Coman katika mchezo huo.

Besiktas ilicheza pungufu ikiwa na wachezaji 10, baada ya beki Domagoj Vida kulimwa kadi nyekundu na mwamuzi Ovidiu Hategan wa Romaniakwa utovu wa nidhamu.