Kipa Denmark asononeka kuwakosa mashabiki Ireland

Muktasari:

Ireland imepoteza nafasi ya kucheza fainali hizo kutoka barani Ulaya na tayari mataifa kadhaaa yameshafuzu.

KIPA wa timu ya taifa ya Denmark, Kasper Schmeichel amesema kuwa kwa mara ya kwanza watawakosa mashamsham ya mashabiki wa Ireland katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia.

Ireland imepoteza nafasi ya kucheza fainali hizo kutoka barani Ulaya na tayari mataifa kadhaaa yameshafuzu.

Mataifa yaliyofuzu kutoka Ulaya ni wenyeji Russia, Ubelgiji, Croatia, Denmark,

England, Ufaransa, Ujerumani, Iceland, Poland,Ureno, Serbia, Hispania, Sweden na 

Switzerland.

Schmeichel alisema kuwa kila mara kumekuwa na mashabiki wa Ireland wanaotia chachandu fainali za Kombe la Dunia.

"Kwa mashindano, ni aibu kuona mashindano yanafanyika bila kuwepo mashabiki wa Ireland...huwa wanachangamsha kweli," alisema Schmeichel.