Fellaini awachukulia poa walioposti picha yake ya kiajabu

Wednesday August 9 2017

 

Mashabiki mtandaoni wametuma picha ya Marouane Fellaini yenye mwonekano wa ajabu ikifananisha na ile wakati akipiga mpira kwenye mechi ya jana Jumanne dhidi ya Real Madrid.

Mchezaji huyo aliwajibu mashabiki wake waliotengeneza picha hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter  akionyesha kufurahishwa licha ya kuongezewa vionjo.

Picha hiyo iliwekwa kwenye muonekano tofatauti zikiwamo iliyowekwa mshumaa ukiyeyuka juu ya kichwa, nyingine ni ile ya kinyago iliyofanana kama aliyowahi kutengenezewa Cristiano Ronaldo.