Eti Melissa Satta hamjui Ronaldo

Muktasari:

Mrembo Melissa, ambaye aliwahi kuwa gumzo baada ya kufichua kwamba Boateng haponi majeraha yake kwa sababu amekuwa akihusudu sana ngono, wakifanya mara 10 kwa wiki, safari hii ametoa mpya baada ya kuuliza, kwani Cristiano Ronaldo ndio nani.

SUPASTAA, Kevin-Prince Boateng huko aliko lazima atakuwa anatembea kifua mbele baada ya kumsikia mrembo wake, Melissa Satta akionyesha kwamba hababashwi na mbwembwe nyingi za Cristiano Ronaldo.

Mrembo Melissa, ambaye aliwahi kuwa gumzo baada ya kufichua kwamba Boateng haponi majeraha yake kwa sababu amekuwa akihusudu sana ngono, wakifanya mara 10 kwa wiki, safari hii ametoa mpya baada ya kuuliza, kwani Cristiano Ronaldo ndio nani.

Ronaldo, ambaye hivi karibuni alikamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Juventus kwa ada ya Pauni 99 milioni, leo Jumapili anatarajia kumenyana na Sassuolo kwenye Serie A.

Melissa, ambaye alioana na Boateng, aliyewahi kuichezea Tottenham Hotspur, aliulizwa kama anamfikiriaje Ronaldo atakapopambana na timu anayochezea kipenzi chake huyo, ndipo hapo mrembo huyo alipotoa kali, aliposema: “Cristiano ndio nani?”

Kisha akaongeza: “Siku zote macho yangu mie yapo kwa Boateng.”

Ronaldo hadi sasa amecheza mechi tatu kwenye Serie A na bado hajafunga bao lolote tangu alipojiunga na Juventus akitokea Real Madrid kwenye dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi huko Ulaya.