Eti Emery anataka kumpiga bei Lacazette

STRAIKA wa Arsenal, Alexandre Lacazette ameripotiwa kuwekwa kwenye rada za Fenerbahce ya Uturuki na huenda kocha mpya wa timu hiyo ya Emirates, Unai Emery anaweza kukubali kumpiga bei. Kumekuwa na madai Kocha Emery hampigii sana hesabu mshambuliaji huyo wa Kifaransa hivyo atakuwa tayari kupokea ofa yoyote itakayomhusu mchezaji huyo.

Taarifa za kutoka Uturuki zinadai Fenerbahce wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Lyon ili akashirikiane na mkali wa zamani wa Tottenham, Roberto Soldado. Ripoti zinadai Emery anataka kumbadili Lacazette na mshambuliaji wa Valencia, Rodrigo aliyewahi kuichezea Bolton kwa mkopo amefunga mabao 19 La Liga msimu uliopitana.

Hata hivyo, bado hakuna uhakika kama Lacazette ataondoka akiwa ametua kwenye timu hiyo mwaka jana tu kwa Pauni 46.5 milioni.