Real Madrid kuna nini? Mwingine achunguzwa tuhuma za ukwepaji kodi

Muktasari:

Wachezaji Cristiano Ronaldo na Luka Modric ni miongoni mwa waliotuhumiwa na mamlaka ya kodi Hispania.

Hispania. Mchezaji wa Real Madrid, James Rodrigues ameungana na wachezaji wa wawili wa timu hiyo na kocha wa zamani Jose Mourinho kwenye sakata la ukwepaji kodi.

Wachezaji Cristiano Ronaldo na Luka Modric ni miongoni mwa waliotuhumiwa na mamlaka ya kodi Hispania.

Rodriguez anatuhumiwa kukwepa kodi kwa takribani miaka 6 inayokadiriwa kufikia Pauni 63.75 milioni wakati akihama kutokea Monaco baada ya Kombe la Dunia mwaka 2014.

Mashtaka ya mchezaji huyo yanatokana na kudanganya kwenye mkataba wake wa awali ambao ulionyesha hatakuwa akipokea bonasi wala haki za matangazo ya picha lakini ni tofauti na sasa ambapo anapokea takribani Pauni 6.6 milioni.

Mamlaka ya Kodi nchini Hispania imeanza kushughulikia masuala yanayohusiana na ukwepaji kodi kwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani na Cristiano Ronaldo atapanda kizimbani Julai 31.