Essien mbioni kutimkia Croatia

Muktasari:

Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea amekuwa nje ya uwanja tangu alipoachana na Panathinaikos mwaka jana Agosti.

Michael Essien yuko mbioni kutimkia Croatia kucheza soka la kulipwa katika klabu ya HNK Rijeka.


Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea amekuwa nje ya uwanja tangu alipoachana na Panathinaikos mwaka jana Agosti.


Kwa mujibu wa Radio Rijeka, imeripoti kuwa kiungo mwenye miaka 34, yuko mbioni kujiunga na klabu hiyo kutoka pwani ya Adriatic.

HNK Rijeka kwa sasa inaongoza Ligi Kuu Croatia ikiwa pointi sita mbele ya Dinamo Zagreb.

Essien anamatumaini ya kufurahi maisha ya soka ya Croatia kuliko ilivyokuwa Athens.

Mghana huyo maisha yake katika klabu ya Panathinaikos yalitawaliwa na majeruhi ya mara kwa mara.

Essien bado anamwaka moja katika mkataba wake na klabu hiyo ya Ugiriki,  lakini mwenyewe anadai ameachwa kama mchezaji huru.