Yanga ikitolea Tanzania pigo kimataifa

Muktasari:

Mabingwa hao wa Tanzania wanasaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya pili

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamefuzu kwa hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika huku ratiba yake ikataraji kupangwa kesho jijini Cairo, Misri.

Yanga imefuzu kwa hatua hiyo baada ya kutolewa katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa na Township Rollers ya Botswana ikifungwa 2-1.

Yanga inasubiri droo ya kesho ikiwa na lengo moja tu la kurudi rekodi yake ya mwaka 2016, ilipoitoa Sagrada Esperanca ya Angola na kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.

CAF kesho ifanya droo ya hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho huku Yanga ikiomba kutokutana na miamba mingine ya Afrika katika hatua hiyo ili kurudia mafanikio yake ya mwaka 2016 ilipocheza hatua ya makundi.

Timu ambazo zinaweza kukatika ndoto ya Yanga katika hatua hiyo iwapo na SuperSport United (Afrika Kusini), USM Alger (Algeria), El Masry (Misri), Raja Casablanca (Morocco), Enyimba (Nigeria), Hilal El Obied (Sudan), AS Vita (DR Congo), na  Zanaco (Zambia).

Mechi hiyo ya mtoano aina umuhimu kwa Yanga pekee bali kwa klabu zote za Tanzania katika kuhakikisha nafasi ya timu mbili inabaki hasa baada ya KCCA ya Uganda kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa rekodi za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Tanzania ina pointi tano ikiwa nafasi ya 16 kati ya nchi 18 kwenye msimamo ikiongozwa na Misri yenye pointi 85.

Pointi tano za Tanzania zimetokana na Yanga kushiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2016 na kushika nafasi ya mwisho katika kundi lake.

Hata hivyo, pointi hizo zingeweza kupungua mwakani na kubaki tatu, pia zingeongezeka na kufikia 13 endapo Simba na Yanga zingetinga hatua ya makundi msimu huu.

Dua pekee kwa Watanzania ni Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, kinyume na hapo inaweza kuondolewa katika msimamo huo na kupishana na Uganda.

Uganda imepanda baada ya KCCA kushiriki mara mbili ndani ya miaka mitatu na msimu huu ikipenya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itafikisha pointi tisa mwakani.

Yanga endapo itashindwa kutinga hatua hiyo itaiondoa Tanzania katika ubora huo na kuzipa mlima klabu nyingine nchini kubaki na pointi tatu ambazo zitavukwa na mataifa yaliyopo chini yake mwaka huu.

Angola ambayo iko nafasi ya 17 mwaka huu ikiwa na pointi tatu, mwakani itaongeza baada ya kuingiza timu moja katika Ligi ya Mabingwa Afrika 1º de Agosto iliyopata tiketi hiyo baada ya kuitupa nje Bidvest Wits ya Afrika Kusini.

Nchi inayoshika mkia katika ubora ni Ethiopia yenye pointi mbili ambayo inapambana kuhakikisha klabu zake mbili Saint George na Welayta Dicha zinatinga hatua ya makundi ili kuikimbia Tanzania.

Hatma ya Yanga kutinga hatua hiyo itaanza rasmi kesho baada ya Caf, baada ya leo kutolewa ratiba ya mashindano.

Awali, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema wanatarajia kuzungumza viongozi wa klabu za Simba na Yanga kupata mrejesho wa mashindano ya kimataifa.

Rais Karia alisema wanatarajia kupata taarifa za mashindano kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo kabla ya kuchukua hatua.

Kigogo huyo alisema lengo la mkutano huo ni kutafuta njia bora kwa klabu za Tanzania kushiriki vyema na kupata mafanikio katika mashindano ya kimataifa.

Wapinzani wa Yanga katika hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika ni SuperSport United (Afrika Kusini), CR Belouizdad (Algeria), USM Alger (Algeria), CARA (Congo), CS La Mancha (Congo), El Masry (Misri), Deportivo Niefang (Equatorial Guinea), Wollaita Dicha (Ethiopia), Djoliba (Mali), Fosa Juniors (Madagascar), Raja Casablanca (Morocco), RS Berkane (Morocco), Costa do Sol (Msumbiji), Enyimba (Nigeria), Akwa Utd (Nigeria), Hilal El Obied (Sudan),

Waliotoka wote Ligi ya Mabingwa ni Bidvest Wits (Afrika Kusini), ASEC Mimosas (Ivory Coast), Williamsville AC (Ivory Coast), AS Vita (DR Congo), Saint George (Ethiopia), Gor Mahia (Kenya), CF Mounana (Gabon), Aduana Stars (Ghana), UD Songo (Msumbiji), MFM FC (Nigeria), Plateau United (Nigeria), Rayon Sports (Rwanda), Generation Foot (Senegal), El Hilal (Sudan), na Zanaco (Zambia)