Ushamba wamsaidia Manula kimtindo aisee

Aishi Manula

Muktasari:

  • Manula, alisema inawezekana wenye tabia hiyo mbaya ya kupanga matokeo wanashindwa kumvaa kwa vile hanma mazoea ya kujichanganya na watu hasa maeneo ya starehe, hivyo ni ngumu kumshawishi.

KIPA namba moja wa timu ya taifa, Taifa Stars na Simba Aishi Manula amefichua kuwa, hawajahi kufuatwa na viongozi wa timu pinzani ili kumshawishi auze mechi na wala hajafikiria kufanya upuuzi huo kwa kuamini utachangia kushusha heshima yake.

Manula, alisema inawezekana wenye tabia hiyo mbaya ya kupanga matokeo wanashindwa kumvaa kwa vile hanma mazoea ya kujichanganya na watu hasa maeneo ya starehe, hivyo ni ngumu kumshawishi.

“Ushamba wangu nadhani ndio unafanya watu wanaogopa kunifuata kunilaghai ili niuze mechi kwa kunipa pesa lakini nahisi unanisaidia maana kuuza mechi kunashusha hadhi ya mchezaji,” alisema Manula.

Katika hatua nyingine Manula, alisema wachezaji wengi wa soka nchini hawana elimu ya kutosha na ndio sababu zinazopelekea kushindwa kuweka watu maalumu wa kuwasimamia hasa katika masula ya sheria na usimamizi wa fedha.

“Wachezaji wengi wanaishi kwa mazoea na wengine kutokuwa na elimu na kuwa chjini ya meneja anaoka kazi kwa sababu ya kutakiwa kumlipa mashahara ama mgawanyo wa asilimia kwa kile anachokiingiza, hili ni tatizo,” alisema.

Manula alisema kusimamiwa na meneja ni jambo nzuri na inasaidia kuongeza thamani ya mchezaji husika kwasababu hupunguza baadhi ya majukumu ambayo ni nje ya uwa nja na hasa suala la kuisoma na kuielewa mikataba yenye manufaa kwao.