Ubinafsi wa Ronaldo hauniumizi kichwa

Monday November 13 2017

 

Madrid, Hispania. Mshambuliaji Karim Benzema amesema Cristiano Ronaldo ni mbinafsi kuliko yeye, lakini hiyo ni kawaidia.

 Mapumziko mengine ya mechi za kimataifa yanashudia mshambuliaji Karim Benzema akiendelea kuachwa katika kikosi cha Didier Deschamps, wakati katika ligi yeye na Cristiano Ronaldo wakipoteza uwezo wa kufunga katika ligi.

Wakati Real Madrid ikiwa na kibarua cha kufukia tofauti ya point inane na Barcelona, imeanza kuonyesha kuwa Benzema anatafuta kurudi katika ubora wake haraka iwezekanavyo.

"[Ronaldo] ni mchoyo kuliko mimi, lakini hiyo ni kawaida," alisema Benzema katika mahojiano yake na Canal.

"Tunaishi vizuri, napenda kucheza naye.

"Mwisho wa siku, ubinafsi wake haunipishida, ni mzuri kwa timu," alisema Benzema.