Traore akimbia benchi Chelsea ajifunga Lyon

Paris, Ufaransa. Mshambuliaji wa Burkina Faso, Bertrand Traore amekamilisha usajili wake kutoka Chelsea na kujiunga na Olympique Lyonnais ya Ufaransa.

Klabu huyo ilitangaza kumsajili chipukizi huyo mwenye miaka 21 kwa mkataba utakaodumu hadi 2022. Gharama ya uhamisho wake ni euro10-milioni.

Traore, alisajiliwa Blues mwaka 2013, lakini ameshindwa kupenya katika kikosi cha  Stamford Bridge, na misimu ya karibuni alipelekwa kwa mkopo katika klabu za Uholanzi za Vitesse Arnhem na AFC Ajax.

Msimu uliopita alisaidia Ajax kucheza fainali ya UEFA Europa Ligi, pamoja na kuonyesha kiwango cha juu zaidi dhidi ya Lyon katika nusu fainali.

“Wakati nilipokuja hapa na Ajax miezi michache iliyopita, nilivutiwa na falsafa ya klabu huu, ikiwa na wachezaji wengi chipukizi kutoka katika academy yao ya Parc OL. Ni sawa Ajax, inayotumia mfumo huo ndiyo jambo lililonivutia hapa,” Traore aliimbia OLTV.