Soka la ukumbini kwa njia ya freestyle latua Afrika

Muktasari:

  •  Mchezo huo ambao huhusisha utumiaji wa viungo tofauti vya mwili kuchezea mpira wa miguu, ulipata bingwa wa kwanza barani Afrika mwishoni mwa wiki nchini Nigeria.

 Dar es Salaam. Wengi wamezoea kuona mchezo wa soka ukichezwa uwanjani, lakini huu wa kucheza ukumbini sasa ni mpya na tayari mashindano ya kimataifa barani Afrika yamefanyika kwa mara ya kwanza jijini Lagos, Nigeria.

Fainali za mashindano ya kwanza ya ubingwa wa Afrika ya mchezo huo, maarufu kwa jina la Freestyle Football, zilifanyika Jumamosi wakatio mshindani kutoka Ivory Coast alitwaa ubingwa na kujinyakulia kitita cha dola 3,000 za Kimarekani ambazo ni sawa na takriban Sh6.3 milioni za Kitanzania.

Mchezo huo huhusiaha uwezo wa mshindani kuchezea mpira kwa viungo vyake vyote isipokuwa kuushika kwa mikoni. Mshindano huweza kuchezea mpira kwa kupiga danadana za miguu, kichwa mapega, kuubana miguuni na kupinduka nao kwa njia ya sarakasi na mwembwe nyingine na baadaye majaji kuamua mshindi.

Hayo yote hufanyika juu ya jukwaa ambalo huwekwa ukumbini kuwezesha mashabiki kushuhudia vipaji tofauti vya washindani.

Akiongea na shirika la habari la AFP, mshindi wa kwanza wa mashindano hilo, Ben Abdul Nader Kone alisema ushindi wake utakuwa mfano kwa vijana wengine.

 

SOUNDBITE 1 :

"Kama Mwafrika ni muhimu kwangu kwa sababu nimeshapoteza fursa nyingi. Kwa hiyo naweza kuwa mfano kwa watoto wengi, vijana wengi ambao wanataka kufanya kitu kama mimi na ni kitu kinafurahisha kweli."

Mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo, valendine Ozigbo, ambaye ni mwenyekiti wa taasisi ya Feet and Tricks International, alisema lengo lao la kuhakikisha wanakidhi kiu ya kupata furaha vijana, limefanikiwa.

 

SOUNDBITE 2:

"Kitu chochote kinachoweza kuweka furaha usoni mwa watu, chochote kinachowezesha vijana, chochote kinachoweza kuwafanya watu wawe na utimamu wa mwili na wenye afya, chochote kinachoweza kuweka fedha mezani ili watu wazipate na kuwa huru, chochote kinachoweza kuleta furaha duniani, ninakifanya na mashindano haya ni mfano wake".

Naye mkurugenzi wa taasisi hiyo, Odyke Nzewi alisema amefurahia kuwa wamefanikiwa kuikusanya Afrika nchini Nigeria kwa kutumia kitu walichokianzisha muda miezi michache iliyopita.

 

SOUNDBITE 3:

"Tulianza mradi huu mwaka jana wakati tulipokuwa na mashindano ya kwanza ya ubingwa wa Nigeria wa Freestyle Football, na tulikuwa na mshindi kwa wanaume na wanawake. Mwaka huu, tulikuwa tunatarajia kuwa na mashindano mikoani na baadaye kuwa na fainali kubwa, kabla ya shirikisho la dunia la Freestyle Football kutuuliza kama tunaweza kuandaa mashindano ya ubingwa wa Afrika. Kwa hiyo tuna furaha kwamba tumeweza kuileta Afrika nchini Nigeria kwa kitu ambacho tulianzisha mwaka jana tu."