Simba yaamua kuweka kambi Afrika Kusini

Friday July 21 2017

 

Dar es Salaam. Washindi wa Kombe la FA, Simba wataondoka nchini keshokutwa Jumanne kwenda Afrika Kusini kwa maandalizi ya msimu mpya.

Simba imejizatiti kufanya vizuri kwenye msimu mpya, hivyo imepanga kuwa na maandalizi ya maana nchini humo na itarejea nchini siku chache kabla ya maadhimisho ya Simba Day, Agosti 8 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, imesema Simba ikiwa Sauzi itacheza mechi za kirafiki ili kocha Joseph Omog aweze kuona upungufu uliopo na kuufanyia kazi.