Shekhan akubali usajili wa Okwi utaibeba Simba kimataifa

Muktasari:

  • Simba inaimarisha kikosi chake kutokana na kukabiliwa na mashindano ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Simba itaiwakilisha nchi mwakani.

Wakati mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi akikamilisha usajili wa kujiunga na Simba, kiungo wa zamani wa Simba Shekhan Rashid amesifu usajili huo.

Simba inaimarisha kikosi chake kutokana na kukabiliwa na mashindano ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Simba itaiwakilisha nchi mwakani.

Akizungumza kutoka nchini Sweden, Shekhan alisema usajili huo utaongeza chachu kwenye kikosi cha Simba katika idara ya ushambuliaji.

“Okwi hajaisha kama watu wanavyoamini, wachezaji wana vipindi, kuna wakati wanashuka na kuna wakati wanapanda. Huyu ni mchezaji aliyekomaa,”alisema Shekhan,aliyeichezea Simba mwanzoni mwa 2000

Aliongeza kuwa ukomavu wa Okwi katika mechi za kimataifa utakuwa na manufaa kwenye kikosi cha Simba kwenyemashindano mbalimbali msimu ujao.