VIDEO: Nitabeba mikoba ya Okwi: Salamba

Muktasari:

Salamba amejiunga na Simba akitokea Lipuli ya Iringa na ameongezwa kwenye kikosi cha Simba mjini hapa kwaajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup.

Nakuru. Mshambuliaji mpya wa Simba, Adam Salamba amekiri kuwa kukosekana kwa mastaa wawili wa timu hiyo, Emmanuel Okwi na John Bocco ni changamoto kwao, lakini atapambana kubeba mikoba yao.

Salamba amejiunga na Simba akitokea Lipuli ya Iringa na ameongezwa kwenye kikosi cha Simba mjini hapa kwaajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup.

Simba inacheza fainali hiyo Jumapili dhidi ya Gor Mahia, straika huyo anatarajiwa kuanza kwa mara ya kwanza baada ya kuingia akitokea benchi kwenye mechi iliyopita dhidi ya Kakamega Homeboys.

"Changamoto kwetu kuwakosa mastraika hao wawili, lakini tutabeba mikoba yao. Mchezaji dhamira yangu ni kupambana na kufanya vizuri zaidi, ikiwemo kufunga," alisema Salamba.