Riyad Mahrez aitosa Roma asajiliwe Arsenal

Muktasari:

  • Winga huyo ameshatangaziwa dau  la Pauni 35 milioni na Arsene Wenger hivyo ataendelea kuitumia klabu yake ya Leicester ili kusubiri msimu mwingine wa usajili.

London, England. Nyota wa Leicester City, Riyad Mahrez amegairi kusajiliwa na AS Roma na badala yake anangojea dirisha lijalo la usajili ili kwenda kuichezea Arsenal.

Winga huyo ameshatangaziwa dau  la Pauni 35 milioni na Arsene Wenger hivyo ataendelea kuitumia klabu yake ya Leicester ili kusubiri msimu mwingine wa usajili.

Mahrez ambaye ni raia wa Algeria, awali alisema anataka kuondoka England msimu huu ili kupata changamoto mpya sehemu kwingine na klabu ya Roma ndiyo iliyokuwa akihusishwa kwa kipindi kirefu kwenda kuichezea.