Rada za Wenger zamgeukia kiungo Mreno Carvalho

Muktasari:

  • Wenger anatajwa kutenga Pauni 27 milioni ili kuhakikisha mchezaji huyo anatua kwenye dimba la Emirates msimu huu wa usajili.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameripotiwa kuwa  anajiandaa kufanya usajili wa Mreno, William Carvalho kutoka klabu ya Sporting Lisbon.

Wenger anatajwa kutenga Pauni 27 milioni ili kuhakikisha mchezaji huyo anatua kwenye dimba la Emirates msimu huu wa usajili.

Kiungo huyo mwenye miaka 25, awali alikuwa akihusishwa kutua England ambako klabu mbalimbali zilikuwa zikimhitaji, hata hivyo kwa sasa Wenger pekee ndiye amemshikia bango kuhakikisha anamsajili.