Niyonzima azua janga Simba

Muktasari:

  • Niyonzima ataukosa mchezo huo kutokana na kupata kadi mbili za njano katika mechi mbili zilizopita ambapo kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo anatakiwa kukosa mchezo mmoja.

Nakuru. Kiungo Haruna Niyonzima ameondolewa katika kikosi cha Simba kinachocheza fainali ya SportPesa Super dhidi ya Gor Mahia kesho Jumapili.

Niyonzima ataukosa mchezo huo kutokana na kupata kadi mbili za njano katika mechi mbili zilizopita ambapo kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo anatakiwa kukosa mchezo mmoja.

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djouma alisema pamoja na kumkosa kiungo huyo Mnyarwanda, watapambana kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

"Niyonzima ni mchezaji mmoja kati ya 18 waliokuja, kumkosa haiwezi kupunguza nafasi yetu ya kutwaa ubingwa. Tutapamba wachezaji wengine na watafanya vizuri," alisema Djouma.