Mwanza yafunika Michezo ya Umitashumta

Muktasari:

Mwanza iliibuka bingwa baada ya kujizolea makombe sita katika michezo mbalimbali na kuzibwaga chini mikoa 25 iliyokuwa ikishiriki nayo katika michezo hiyo.

Mwanza. Mkoa  wa Mwanza umeibuka bingwa wa jumla wa Michezo ya Umitashumta iliyomalizika jumatano kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza.

Mwanza iliibuka bingwa baada ya kujizolea makombe sita katika michezo mbalimbali na kuzibwaga chini mikoa 25 iliyokuwa ikishiriki nayo katika michezo hiyo.

Mkoa huo ulianza kuchukua kombe la mchezo wa riadha kwa wasichana, wavu kwa wavulana, mpira wa mikono kwa wasichana, netiboli na soka kwa wavulana.

Nafasi ya pili ilienda kwa Mkoa wa Geita ulijinyakulia makombe manne katika michezo ya riadha wavulana, mpira wa mikono wasichana na wavulana na netiboli.

Dar es Salaam ulishika nafasi ya tatu kwa kunyakulia makombe mawili katika michezo ya wavu kwa wavulana kwakushika nafasi ya kwanza na mpira wa Gallball.

Mikoa iliyoshika nafasi tatu za mwisho ni Iringa (26), Ruvuma (25) na Lindi walioshika nafasi ya 24 katika michezo hiyo.