Mwanamuziki Dede afariki dunia

Muktasari:

Dede ambaye kabla ya kujiunga Msondo Ngoma alikuwa kwenye bendi ya Sikinde, alilazwa hospitalini hapo kwa muda mrefu akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Dar es Salaam. Tasnia ya muziki wa dansi imepata pigo baada ya kuondokewa na mwanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, Shabaan Dede aliyefariki katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili leo saa mbili asubuhi.

Dede ambaye kabla ya kujiunga Msondo Ngoma alikuwa kwenye bendi ya Sikinde, alilazwa hospitalini hapo kwa muda mrefu akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Msemaji wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti alithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo na kusema kuwa ni pigo kwao.

"Ni kweli nimepigiwa simu na mtoto wake akinijulisha kuwa mwenzetu amefariki dunia. Ni habari mbaya kwetu na kwa wapenzi wa muziki wa dansi nchini kutokana na mchango wa marehemu."

"Kwa sasa tunaendelea kufanya mawasiliano na wanafamilia ili tufahamu nini kinachoendelea," alisema Kibiriti.