Msuva mbona Kiarabu poa tu

Muktasari:

Staa huyo wa Kitanzania amekuwa akikumbana na wakati mgumu katika suala la mawasiliano kutokana na wachezaji  wa kikosi chake  kuzungumza Kiarabu na Kifaransa.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Difaa El Jadidi, Simon Msuva unaambiwa ameanza kuiva kuyazunguza baadhi ya maneno ya Kiarabu nchini Morocco.

Staa huyo wa Kitanzania amekuwa akikumbana na wakati mgumu katika suala la mawasiliano kutokana na wachezaji  wa kikosi chake  kuzungumza Kiarabu na Kifaransa.

"Kidogo nimeanza kujua kusalimia, sipati shida nikitaka kumsalimia mtu , itafika hatua nitaijua lugha yao kama wangekuwa wanazungumza na Kingereza mbona mambo yangekuwa safi."alisema Msuva.

Hata hivyo, jana Msuva aliiongoza vema timu yake  kupata matokeo ya ushindi mbele ya Rapide Oued Zem kwa  wa mabao 3-1, matokeo hayo  Difaa  imejikusanyia pointi nne  katika  michezo mitatu ya Ligi Kuu nchini humo.