Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Yanga aaga kwa waraka mrefu, akisubiriwa Uarabuni

Muktasari:

  • Kwanza ni kupisha ujio wa benchi jipya la ufundi chini ya Kocha Mkuu mpya, Manqoba Mngqithi na pili ni baada ya kupata fursa mpya nje ya Tanzania.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Matthew Silva ameaga rasmi ndani ya klabu hiyo jambo linaloonekana kuchangiwa na sababu mbili za msingi.

Kwanza ni kupisha ujio wa benchi jipya la ufundi chini ya Kocha Mkuu mpya, Manqoba Mngqithi na pili ni baada ya kupata fursa mpya nje ya Tanzania.

Matthew ameandika waraka mrefu wa kuaga akisema ndoto zake zimetimia.

“Ninaondoka Yanga kwa namna ambavyo siku zote nilikuwa nikiota. Lengo langu lilikuwa kuondoka nikiwa mtu mwenye utu, mkarimu, mwenye moyo mwema, mwenye nia njema, mchapakazi, aliyejitolea, mwenye shauku, makini, mwenye uwezo na mtaalamu wa kweli. Na kwa furaha kubwa, lengo hilo limetimia.

“Ni kwa misingi hiyo pekee tuliweza kuwa na ndoto na dhamira ya kumaliza msimu tukiwa mabingwa wa kihistoria kwa mara ya tano mfululizo.

“Kwa mara nyingine, kocha Pedro Soares Gonçalves, asante sana kwa kunipa nafasi ya kufanya kazi pamoja nawe katika klabu hii ya kipekee. Imekuwa kipindi cha ajabu sana kuwa hapa, na tumefanya kazi kubwa pamoja, hasa ukizingatia kwamba miaka 20 iliyopita nilikuwa miongoni mwa wachezaji uliowahi kuwafundisha,” amesema Matthew.

Matthew ameishukuru klabu hiyo kwa namna imekuwa ikisapoti benchi la ufundi.

“Kwa viongozi wote wa klabu na timu nzima inayofanya kazi kila siku bila kuchoka kuhakikisha klabu inaendelea kupiga hatua kwa kasi kubwa na kuweka mazingira bora ya kupigania malengo makubwa, asante sana.

“Kwa benchi lote la ufundi na makocha wote ambao mmejitolea na kupambana kila siku ili kuhakikisha historia inaandikwa kupitia kujituma kusikochoka na kazi kubwa inayofanyika nyuma ya pazia kwa heshima na weledi, nawashukuru sana.

“Kwa wachezaji wote ambao walikuwa na hamasa, ubora na dhamira ya kutimiza haya yote uwanjani katika kila mechi, huku mkibeba jukumu kubwa na kutambua ugumu wa safari hii, nawatakia kila la heri katika maisha na taaluma zenu za soka.

“Na mwisho kabisa, kwa Wananchi wote popote mlipo. Msaada wenu hauna kikomo, Haujaenea tu kila kona ya Tanzania, wala Afrika Mashariki pekee kama klabu kubwa na bora zaidi, wala Afrika tu, bali umefika duniani kote,” amesema Matthew.