Messi, Suarez na Neymar miaka minne pamoja

Friday July 21 2017

 

Barcelona, Hispania. Msimu wa 2017/18, ni msimu wa kwanza kati ya minne kwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar (MSN) kuanza pamoja tangu siku ya kwanza ya mazoezi ya timu hiyo.

Katika misimu mitatu iliyopita, nyota hao walikuwa wakipewa muda zaidi wa kupumzika kutokana na kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa kuanzia Kombe la Dunia, Copa Amerika pamoja na Michezo Olimpiki.

Sasa kocha mpya wa Barca, Ernesto Valverde, na nyota hao wa Amerika Kusini watapata moda wa kujifunza mbinu mpya pamoja tangu mwanzo wa msimu.

Hiyo ni tofauti ilivyokuwa wakati wa Luis Enrique aliyechukua jukumu hilo 2014, msimu ambao Suarez aliamia Camp Nou.

Si kazi rahisi kuipangua safu ya ushambuliaji wa MSN ambayo katika misimu mitatu wamefunga mabao 363 chini Luis Enrique, hivyo msimu huu nyota hao wanategemea kuendelea kuibeba Barcelona.