Mchongo wa Msuva hivi buana!

Muktasari:

Msuva ametua nchini baada ya Ligi Kuu Morocco ‘Batola Pro’ kumalizika huku klabu yake ikiukosa ubingwa kwa kushika nafasi ya tano.

MSHAMBULIAJI wa Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva, aliyewasili nchini jana kwa mapumziko, amesema ugumu wa ligi ya nchi hiyo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa uwezo wake.

Msuva ametua nchini baada ya Ligi Kuu Morocco ‘Batola Pro’ kumalizika huku klabu yake ikiukosa ubingwa kwa kushika nafasi ya tano.

Pamoja na Difaa kushika nafasi hiyo, Msuva ameonekana kung’ara kwenye msimu wake wa kwanza tu akifunga mabao 11 ambayo yamemfanya kuwa kinara wa mabao ndani ya klabu hiyo.

“Ugumu wa ligi umechangia kuwa kwenye hiki kiwango, kwa kiasi kikubwa nilichopanga kwenye msimu wangu wa kwanza kimetimia na nashukuru sana wenzangu kule kwa kunipa ushirikiano wa kutosha,” alisema.

“Bado nina safari ndefu mbele, nitaendelea kupambana mpaka kieleweke. Tulikuwa na nafasi ya kuchukua ubingwa ila tuliteleza kwenye mechi za mwishoni.”