Maxime atuliza mzuka Kagera

Muktasari:

  • Maxime alisema kila timu iliyopo Ligi Kuu inacheza ili kupata matokeo mazuri hivyo hawezi kulaumu wachezaji wake kwa matokeo

Dodoma. Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuanza vibaya kwa timu yake si kigezo cha kushindwa kumaliza katika nafasi tatu za juu za Ligi Kuu Bara msimu huu.

Maxime alitoa kauli hiyo baada ya timu yake kupokea kipigo cha tatu msimi huu kutoka kwa kwa Singida United kwa kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Maxime alisema kufanya vibaya kwenye mechi za awali za ligi kuu siyo sababu ya kuamini hawatofanya vema.

Maxime alisema kila timu iliyopo Ligi Kuu inacheza ili kupata matokeo mazuri hivyo hawezi kulaumu wachezaji wake kwa matokeo waliyoyapata katika mechi za mwanzo wa ligi badala yake watajipanga kwaajili ya kushinda mechi zijazo.

“Ni kweli nimepoteza mechi tatu na sare 1 katika mechi nne tulizocheza na ndivyo mpira ulivyo kila timu inayocheza ligi inacheza ili ipate matokeo hivyo kupoteza huko siyo sababu ya kukata tamaa badala yake tunajipanga kwa mechi zijazo naamini tutafanya vizuri,”alisema Maxime