Marufuku Barcelona na Manchester City kumrubuni Alli

London, England. Ofisa Mkuu wa Tottenham, Daniel Levy ametangaza marufuku klabuni hapo ya kumuuza mshambuliaji wao, Dele Alli kwa gharama yoyote ile hata likitangazwa dau la Pauni 150 milioni kutoka klabu za Barcelona na Manchester City ambazo zinamuwinda.

Mashabiki wa klabu hiyo nao wameingiwa hofu baada ya kuwapo taarifa za mshambuliaji Danny Rose kutaka kutimkia Cheslea katika dirisha la usajili la kiangazi kabla halijafungwa.

Alli mwenye miaka 21 amekuwa miongoni mwa wachezaji chipukizi duniani, huku klabu vigogo barani Ulaya zikimuwinda kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 31.