Lukaku atabiriwa kuvunja rekodi ya Rooney Man United

Sunday September 10 2017

 

Kigogo wa Stoke City, Mark Hughes amemtabiria Romelu Lukaku ana nafasi ya kuvunja rekodi ya mabao ya Wyne Rooney.

Bosi huyo wa Stoke alisema, raia huyo wa Ubelgiji ameonyesha kiwango baada ya kufunga mabao matatu mpaka sasa kwenye Ligi Kuu England.

Rooney alifanikiwa kuweka nyav uni mabao 263 aiwa na Manchester na kuvunja rekodi iliyowahi kuwekwa na mkongwe Sir Bobby Charton klabuni hapo kwa kufunga mabao 163 enzi hizo.