Liverpool yaweka dau la kufuru kwa kipa Roma

Muktasari:

  • Liverpool haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England tangu 1990

London, England. Liverpool imeweka meza dau la pauni 62 milioni ili kumnasa kipa wa Roma, Mbrazilia Alisson.

Roma wapo tayari kupokea dau hilo na kuvunja rekodi ya uhamisho wa kipa, lakini watakuwa tayari kuwamwachia iwapo watapewa pauni 66milioni.

Alisson hivi karibuni alikuwa na kikosi cha Brazil kilichotolewa katika robo fainali ya Kombe la Dunia Russia.

Kipa huyo mwenye miaka 25, amekuwa Roma kwa miaka miwili akitokea katika klabu ya Brazil ya Internacional.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alilazika kumtetea tena kipa wake Loris Karius wiki iliyopita kutokana na kufanya makosa ya kizembe katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Tranmere.

Kipa huyo Mjerumani mwenye miaka 25, alifunga bao la mpira wa adhabu na kusababisha wenyeji kupata goli katika ushindi wa Liverpool 3-2 kwenye Uwanja Prenton Park.

Karius alifungwa mabao mawili ya kizembe wakati Liverpool ilipochapwa 3-1 na Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.