Ligi ya netiboli kupigwa Arusha

Muktasari:

Mwenyekiti wa chama cha netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibira alisema wameamua kuwapa Arusha kutokana na sababu mbalimbali moja wapo ni kuwa na timu tatu zinazoshiriki ligi hiyo ambazo ni Polisi, Madini na Arusha Queen.

Arusha: Mkoa wa Arusha umepewa dhamana ya kuandaa ligi daraja la kwanza netiboli itakayoanza Septemba 13 hadi 26 mwaka huu.

Mwenyekiti wa chama cha netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibira alisema wameamua kuwapa Arusha kutokana na sababu mbalimbali moja wapo ni kuwa na timu tatu zinazoshiriki ligi hiyo ambazo ni Polisi, Madini na Arusha Queen.

“Maandalizi yanaendelea vizuri Arusha pamoja na kuzitaka timu zote 21, zinazoshiriki ligi hiyo  kuanza kujiandaa kwa msimu mpya wa ligi” alisema Kibira.

Kibira aliwaomba wadau mbalimbali kuwaunga mkono ili kufanikisha ligi hiyo.