Kuna mastaa tisa wanakatwa huko Arsenal

Muktasari:

Kutokana na timu hiyo kupambana na hali yake Ligi Kuu England, inaonekana bayana itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo, na sasa ni wazi kutakuwa na panga kubwa kuondoa wachezaji wasiostahili kuendelea kuichezea timu hiyo yenye maskani yake Emirates.

LONDON,ENGLAND

ARSENAL imeripotiwa itakuwa bize kweli kweli mwishoni mwa msimu huu kufanya usajili wa nguvu kwa sababu kuna mastaa wasiopungua tisa watapigwa chini.

Kutokana na timu hiyo kupambana na hali yake Ligi Kuu England, inaonekana bayana itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo, na sasa ni wazi kutakuwa na panga kubwa kuondoa wachezaji wasiostahili kuendelea kuichezea timu hiyo yenye maskani yake Emirates.

Orodha hiyo ya wachezaji imedaiwa kumhusu pia beki wa pembeni, Mhispaniola Hector Bellerin, ambaye Arsenal wamedaiwa wapo tayari kumpiga bei Man United au Barca ambako anatakiwa kwa nguvu zote. Wengine ni Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Calum Chambers, David Ospina, Danny Welbeck, Lucas Perez, Joel Campbell na Carl Jenkinson.

Arsenal itahitaji kuwekeza kwenye kikosi chao katika msimu wa mwisho wa Arsene Wenger ili kuhakikisha wanampa nafasi kocha huyo kusaini ‘out’ kwa mafanikio ya kunyakua moja ya mataji makubwa kabisa kikosi hapo.