Kiungo wa Chelsea Tiemoue Bakayako apata ajali

Muktasari:

  • Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya kutoka uwanjani wakati akirejea nyumbani.

 Kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko amepata ajali jana Alhamisi jioni wakati akitoka mazoezi huku sababu ikielezwa kuwa ni kutokana na kushindwa kumudu mfumo wa kuendesha upande wa kushoto.

Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya kutoka uwanjani wakati akirejea nyumbani.

Polisi walifika eneo la tukio ilipotokea ajali hiyo mita chache kutoka uwanja wa mazoezi wa Chelsea kisha kutoa msaada.

Hata hivyo, kiungo huyo hajapata majeraha yoyote kutokana na ajali hiyo na kocha Antonio Conte alisema amepata taarifa kuhusu ajali hiyo na kumpa pole mchezaji wake.

 Taarifa zaidi zitatolewa leo Ijumaa kwenye mkutano wa kocha huyo na waandishi wa habari.