Himid: Stars itashinda Rwanda

Muktasari:

Nahodha wa timu hiyo, Himid Mao alisema bado wana nafasi katika mechi ya marudiano, hivyo Watanzania wawaunge mkono ili waweze kuvuka hatua nyingine mbele.

Dar es Salaam. Sare ya Stars dhidi ya Rwanda katika mashindano ya CHAN, ilionekana kuwavunja moyo Watanzania, lakini nyota wa kikosi hicho wamewakumbusha wadau wa soka nchini, kuwaunga mkono kwa madai safari inaendelea.

Nahodha wa timu hiyo, Himid Mao alisema bado wana nafasi katika mechi ya marudiano, hivyo Watanzania wawaunge mkono ili waweze kuvuka hatua nyingine mbele.

"Tunacheza Jumamosi ya Julai 22, hivyo mashabiki wasikate tamaa, sote tunatamani kuona tunapiga hatua ya maendeleo ya mpira wa miguu nchini na mpira ni matokeo uwanjani hivyo haijalishi ni kucheza ugenini."

Mao alisema kilichowakatisha tamaa Watanzania ni kutoka sare nyumbani na kwamba hawaaamini kama wanaweza kupata ushindi ugenini kitu alichosema si jambo jema kukata tamaa kwani vita ni kupambana.