Garbine Muguruza amfyatua Venus Williams na kutwaa ubingwa wa tenisi Wembledon 2017

Friday July 21 2017

 

London, England. Garbine Muguruza ametibua rekodi ya Mmarekani, Venus Williams baada ya kumfunga kwa seti 7-5 na 6-0 kwenye fainali ilipigwa leo Jumapili katika mashindano ya tenisi upande wa wanawake Wembledon.

Baada ya ushindi huo Muguruza amepanda kwenye viwango vya dunia na kufikia namba tano duniani ambavyo vitatangaza rasmi kesho Jumatatu.

Mchezaji tenisi huyo mwenye miaka 23 awali, alifanikiwa kutwaa pia taji la ubingwa la Grand Slam pia alishinda mashinano ya wazi ya tenisi maarufu French Open.